SIMBA KAZINI LEO KIMATAIFA

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho wakiwa hatua ya makundi Simba wana kazi ya kusaka pointi tatu mbele ASEC Mimosas.

Huu ni mchezo wa tano kwa Simba wakiwa na pointi 7 kibindoni baada ya kucheza mechi 4 na wapinzani wao ASEC Mimosas wapo nafasi ya pili na pointi 6.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 3-1 hivyo leo wapinzani wao watakuwa na hesabu za kupindua meza kibabe.

Hautakuwa mchezo rahisi kwa kuwa katika mashindano haya inaonekana kwamba kila timu inatumia vema faida ya mechi za nyumbani.

Pablo Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanahitaji ushindi katika mchezo wa leo.

“Tupo ugenini na wapinzani wetu wanahitaji ushindi hasa ukizingatia kwamba mchezo wa kwanza tulishinda tukiwa nyumbani.

“Wachezaji wanajua kwamba sio kazi rahisi lakini ambacho kinahitajika ni ushindi, “.