MAPUMZIKO:ASEC MIMOSAS 2-0SIMBA

UBAO unasoma ASEC Mimosas 2-0 Simba na utulivu kwa Simba tatizo dk 14 za mwanzo walitengeneza nafasi nne zote wakakosa na ni shuti moja la Meddie Kagere lililenga lango dk ya 27.

Aubin Kramo Kouame dk 16 na Stephane Aziz wamemtungua Manula ambaye aliokoa penalti dk ya 36.

Simba ina kazi kubwa ya kuweza kusaka ushindi kwa kuwa kundi D mambo sio mepesi kutokana na kila timu kuwa na nafasi ya kuweza kutinga hatua ya robo fainali.

Kiungo Pape Sakho yupo ndani lakini mabeki wa ASEC wamekuwa naye kwa umakini kwa kuwa wanakumbuka ambacho alikifanya Uwanja wa Mkapa kwa kuwa alifunga bao kwa mtindo wa Acrobatic.