MAPUMZIKO:YANGA 1-0KMC, UWANJA WA MKAPA

NI moja ya mchezo bora wa Ligi Kuu Bara ndani ya Machi 19,2022 ikiwa ni mapumziko ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 1-0 KMC.

Bao la kujifunga la Dante dk 39 katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Fiston Mayele.
Yanga wamenyimwa penalti dk 16 na KMC wamenyimwa kona dk 44.

Kasi ya KMC ilikuwa bora kipindi cha kwanza huku umakini ukiwa ni tatizo kwa umaliziaji kwa nyota wa KMC.

Djuma Shaban amekuwa na kazi ya kumwaga maji mbele akimsaka Fiston Mayele mwenye mabao 10 kibindoni na pasi 3.

Ni asilimia 53 za umiliki wa asilimia 47 na Diarra Djigui na Juma Kaseja wamefanya kazi kubwa kulinda malango yao.