BAADA ya kuwasili leo Benin kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya ASEC Mimosas, kikosi cha Simba kimeanza mazoezi.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Machi 20,2022 ni wa hatua ya makundi, Simba ikiwa na pointi 7 huku ASEC 6 ndani ya kundi D.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa ule wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-1 ASEC Mimosas ambapo miongoni mwa waliotupia kwa Simba ni kiungo Pape Sakho.
Pia mabao mengine mawili yalifungwa na Shomari Kapombe na Peter Banda ambaye ni kiungo kinda anayefanya vizuri kwa sasa kila anapopewa nafasi na Kocha Mkuu Pablo Franco.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo.
“Tuna amini kwamba utakuwa mchezo mgumu lakini tupo tayari ili kuweza kupata matokeo kikubwa ni kila mmoja kusubiri na kuona namna tutakavyofanya,”.