KMC YAZIPIGIA HESABU POINTI ZA YANGA

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kwamba hakuna kitakachowazuia kupata matokeo mbele ya Yanga katika mchezo wao wa ligi unaoatarajiwa kuchezwa Machi 19, Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa hakuna kitakachowazuia kupata matokeo mbele ya Yanga.

Christina amebainisha kwamba kupoteza mchezo wao mbele ya Coastal Union kumewapa morali ya kuweza kujipanga kwa ajili ya mchezo wa kesho Machi 19,2022.

“Kitu ambacho kinawezekana ni kwamba mchezo upo kwenye uwezo wetu, tutakuwa ugenini kikanuni lakini tutakuwa nyumbani kwa kuwa tunakwenda kucheza na timu ambayo tunaijua na hakuna kitu ambacho kitatuzuia kupata matokeo.

“Tunakwenda kucheza na timu ambayo inaongoza ligi ukizingatia kwamba tumetoka kupoteza mchezo wetu mbele ya Coastal Union lakini hiyo haitatufanya tuweze kushindwa kupata matokeo mbele ya Yanga.Timu bora haifungwa mara mbili,” amesema Christina.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Majimaji, Songea Yanga iliyo na pointi 45 ikiwa nafasi ya kwanza ilishinda mabao 2-0 dhidi ya KMC iliyo nafasi ya 7 na pointi 22.