VIDEO:MCHAKATO WA MABADILIKO YANGA UPO HIVI

SENZO Mbatha, Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga ameweka wazi kwamba mchakato wa kuelekea kwenye mabadiliko ndani ya timu hiyo unaendelea vizuri na ambacho kipo kwa sasa ni kuweza kukamilisha suala zima la uchaguzi.

Pia amebainisha kuwa jambo ambalo linatazamwa kwa ukaribu kabla ya uchaguzi ni kukamilika kwa usajili wa matawi na wale ambao watakamilisha usajili wao watakabidhiwa vyeti.