PRISONS:BADO TUNATENGENEZA TIMU

SHABAN Kazumba, Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons amesema kuwa bado wanatengeneza timu hivyo wana imani ya kuweza kufanya vizuri kwenye mechi zao zilizobaki.

Ikiwa Uwanja wa Karume, Mara Machi 15,2022 ilikubali kushuhudia ubao ukisoma Biashara United 2-1 Tanzania Prisons.

Ni mabao ya Deogratius Mafie kwa upande wa Biashara United yalipachikwa kimiani dakika ya 26 na 34 huku lile la Prisons likijazwa kimiani na Ezekiel Mwashilindi dakika ya 68.

Kazumba amesema:”Ni kweli tumekuwa tukipata matokeo mabaya ambayo tumepata kwenye mechi zetu za hivi karibuni lakini bado tunajitahidi kutengeneza timu ili kupata matokeo mazuri kwenye mechi zijazo.

“Mashabiki wawe na imani nasi kwani mapambano yanaendelea na tuna amini tutarudi kwenye ubora wetu,” amesema.

Kwenye msimamo Prisons ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi 18 ndani ya ligi msimu wa 2021/22.