IMEKUWA rahisi kwa sasa matukio yote ambayo yanatokea uwanjani kuweza kuonekana baada na kabla ya mchezo hii inatokana na kukua kwa teknolojia.
Weka mbali suala ka kukua kwa teknolojia bado Azam TV wanaonesha kila mechi kuweza kuonyeshwa na mashabiki wakaweza kufurahia burudani.
Mzunguko wa pili umekuwa na matukio mengi ambayo yanatokea yapo mazuri hasa kwa timu ambapo inapata matokeo pamoja na matokeo mabovu pale timu inapopoteza.
Uhalisia katika mpira yote ni matokeo na hakuna timu ambayo inaingia uwanjani ikiwa inajua kwamba itapata nini huu ni ukweli wa mambo na mashabiki wameanza kuelewa na ile tabia ya kubeba matokeo mfukoni imepungua.
Katika mechi za hivi karibuni tunaona kwamba matokeo yanapatikana lakini wachezaji hawapo salama kwa asilimia kubwa kutokana na matumizi makubwa ya nguvu.
Ipo wazi kwamba mpira wa miguu huwezi kuzuia mingongano lakini ni lazima kila mchezaji kuwa mlinzi wa mchezaji mwingine.
Maisha ya mchezaji yanategemea kucheza mpira na pale anapoumizwa inamfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Hakuna namna tulishuhudia matukio haya mzunguko wa kwanza wapo wachezaji ambao waliweza kuumizwa kutokana na kuchezewa faulo wakawa nje kwa muda.
Sasa tumeanza mzunguko wa pili tunaona wachezaji wameanza kuishi maisha ya mzunguko wa kwanza katika hili ni lazima kila mchezaji kuweza kuwa katika hali ya utofauti.
Ni muhimu mchezaji akawa mlinzi wa mchezaji mwingine hii itafanya kila mtu aweze kuonesha kile ambacho anacho kwenye miguu yake.
Wale ambao waliweza kutumia nguvu kubwa na kuumiza wengine tunatambua kwamba haikuwa dhamira yao hivyo kwa mechi zijazo ni muhimu kila mchezaji kuwa makini.
Ulinzi wa mchezaji wa ndani mtu wa kwanza ni mchezaji ambaye anajua namna ya kuingia na kutoka kwa mpinzani wake.
Hii ya kuumizana katika mechi za mzunguko wa pili haifai na sio nzuri kwa afya itapendeza ikiwa kila mchezaji atacheza kwa nidhamu.
Imani yangu ni kwamba kila kitu kinawezekana kikubwa ni kuamini kwamba kila mchezaji jukumu lake ni kucheza na kulinda afya ya mwingine.
Suala la kucheza kwa kukamiana lisipewe nafasi hasa mzunguko huu wa pili ambao ni lala salama kwa kila timu kusaka ushindi.
Vijana wanapambana kusaka ushindi na wachezaji wanakazi ya kufanya kutimiza majukumu yao pia.
Ikiwa kila mchezaji atakuwa anajali afya ya mpinzani wake basi usalama wa mchezaji mwingine utakuwa katika hali nzuri na hili linahitajika kwenye kila mechi.
Rai yangu wachezaji kucheza kiungwana na kwa nidhamu katika mechi zote zilizobaki mzunguko huu wa pili ambao una ushindani mkubwa.
Mlinzi wa kwanza wa mchezaji ndani ya uwanja ni mchezaji mwenzake hivyo muhimu kujali afya na usalama wa mchezaji mwingine.
Hakuna ambaye anapenda kuona mchezaji akiwa ameumia lakini haya yanatotokea yasipewe nafasi mechi zijazo.
Kila kitu kinawezekana na muda wa kuwa mlinzi wa mwingine ni sasa haya ni maisha hivyo tucheze kwa uungwana.