ANAANDIKA Saleh Jembe:-
WAKATI Simba inapoteza 2-0 dhidi ya Berkane kule Morocco, Fiston Abdullazak alikuwa jukwaani kabisa. Wakati Simba ikishinda 1-0 pale kwa Mkapa dhidi ya Berkane, alipata bahati angalau ya kuwa benchi.
Ajabu sana mchezaji huyu ambaye aliachwa na Yanga kutokana na kiwango duni alisajiliwa Berkane (Amini suala la bahati lipo), jiulize vipi timu kama Berkane imsajili mtu kama Fiston huyu na isimsajili Lusajo au George Mpole…..??
Binafsi nimeamua kuandika hapa kuonyesha kero yangu dhidi ya mchezaji huyu ambaye awali niliamini ni profesheno KUMBE LA.
Najua ulimsikia akimponda beki wa kati wa Simba, Joash Onyango na kumuita babu….haikutosha alipotua Dar, ajabu mashabiki zaidi wakajipendekeza kwake, naamini hawakujua hata BENCHI KWAKE NI BAHATI, Naye akajigamba kuonyesha wako tayari kuimaliza Simba utafikiri ana uhakika wa kucheza.
Jiulize Kisinda anayecheza, aliyewahi kumpita Onyango akalazimika kumuangusha mbona hakusema maneno ya KITOTO kama yake….
Haya sasa, WAMEFUNGWA, Simba inawazidi pointi na Kocha Ibenge kakalia kuti kavu, yeye MDOMO wa mchezaji utafikiri shabiki umemsaidia nini?
Naamini hatakuwa na muda mwingi Berkane, Waarabu watang”amua na KUMFUNGASHIA VIRAGO….
Mkimuona muambieni ajifunze WELEDI, ajitofautishe kama mchezaji na shabiki….
Namkumbusha ubora wa mchezaji ni takwimu bora na kama mshambulizi basi afunge au azalishe mabao na MANENO MENGI, AWAACHIE MASHABIKI MAANA HAYACHEKI NA HAYATAMSAIDIA…
THIS IS TANZANIA….??