ATLETICO MADRID YASEPA NA POINTI TATU KWA USHINDI WA MABAO 2-1

ATLETICO Madrid walisepa na pointi tatu mazima mbele ya Cadiz katika mchezo wa La Liga uliochezwa Uwanja wa Wanda Metropolitan.

Mabao ya Joao Felix dk 3 na Rodrigo De Paul dk 68 yalitosha kuwapa pointi muhimu licha ya kukamilisha mchezo wakiwa pungufu baada ya Javi Serrano kuonyeshwa kadi nyekundu dk ya 88.

Bao la Cadiz lilipachikwa kimiani na Alvaro Negredo ilikuwa dk ya 45 halikuweza kuwapa pointi wapinzani hao.

Atletico Madrid inafikisha pointi 51 ikiwa nafasi ya 3 huku Cadiz ikiwa na pointi zake 24 nafasi ya 18.

Vinara ni Real Madrid wakiwa na pointi 63 baada ya kucheza mechi 27.