ROMAN Abramovich na Serikali ya Uingereza imeripotiwa kwamba wamefikia makubaliano kwa ajili ya suala la mauzo ya timu ya Chelsea.
Serikali inaelezwa kuwa inazingatia suala la timu hiyo kuwekwa sokoni ili kuweza kupata matokeo mazuri kwa ajili ya Chelsea.
Kampuni ya Raine Group imeelezwa kuwa imepewa ruhusa ya kuendelea na mchakato wa kusaka mshindani ambaye atachukua timu hiyo.
Hali hiyo imekuja baada ya timu hiyo kuendelea na shughuli zake kama kawaida huku kukiwa na mashaka kuhusu uwezo wa timu hiyo kuweza kumaliza msimu katika hali nzuri.
Kwa mujibu wa The Daily Telegraph imeripoti kwamba pande zote mbili zipo kwenye mpango wa kuweza kufanya usimamizi mzuri.
Alhamisi iliripotiwa kwamba Abramovich alitoa maelekezo ya kusimamisha shughuli zake kutokana na kuhusishwa na ukaribu na Vladimir Putin kuhusu kuendelea na mchakato wa kuiweka timu hiyo sokoni maelekezo hayo inatajwa yalitoka Serikalini.