SIMBA UGENINI WANAPATA MATESO KWELIKWELI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kwa msimu wa 2021/22 wamekuwa wakipata mateso makubwa ugenini katika msako wa pointi tatu kwa kuwa mambo yamekuwa ni magumu kwao.

Kwa mzunguko wa kwanza katika mechi 15 ambazo wamecheza na kuweka kibindoni pointi 31 ni mechi 7 walicheza ugenini na kushinda 3 huku wakiambulia sare 2 na kunyooshwa katika mechi 2.

Ilipoteza mbele ya Mbeya City Uwanja wa Sokoine na ilinyooshwa mbele ya Kagera Sugar kote kipa namba moja Aishi Manula aliokota nyavuni bao mojamoja na waliomtungua ni Amis Kiza wa Kagera Sugar na Paul Nonga wa Mbeya City.

Yanga ni namba moja kwa kushinda ugenini katika mechi 9 ambazo walicheza walishinda mechi 7, sare 2 ilikuwa mbele ya Namungo FC na Simba huku ikiwa haijapoteza kwenye mechi ambazo ilicheza.

Tanzania Prisons wao mechi za ugenini ni mtihani kwao kwa mzunguko wa kwanza kwa kuwa katika mechi 8 walizocheza waliweza kushinda moja, sare 2 na waliambulia kichapo mechi 5.