IMEKUWA ni tofauti kwa yale ambayo walifikiria mashabiki wa Manchester United kuyapata kutoka kwa beki wao wa kazi ambaye ni wa bei ghali.
Bado wapo ambao wanaamini kwamba nyota huyo atarejea kwenye ubora wake na kufanya vizuri kwenye mechi zote za mashindano.
Ni Harry Maguire beki ghali ndani ya Ligi Kuu England mali ya Manchester United ila anachofanya ni tofauti na mkwanja uliokwekwa mezani kumpata.
Manchester United waliweka mezani euro milioni 80 kupata saini ya nyota huyo kutoka kikosi cha Leicester City.
Kutokana na thamani yake aliweza kutumia miezi sita baada ya kuwasili hapo akapewa kitambaa cha unahodha lakini mambo bado.
Toka zama za Ole Gunnar Solskjaer na sasa zama za Ralf Rangnick bado amekuwa akifanya makosa jambo linalowagawa mashabiki.
Maguire amesema:”Yeye, (Rangnick) ameleta matokeo, tunashinda pamoja na kupoteza pamoja. Ubora katika uongozi ni kuweza kuona kwamba timu inamaliza ndani ya nne bora na pia tunahitaji kombe,”.
Licha ya hayo bado mashabiki wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuweza kumlaumu ilikuwa ni kupitia ukurasa wa twitter wa Seth Sithole ambaye alisema kuwa Maguire ni nahodha wa bei ya pauni milioni 80 lakini kiwango chake kinashuka.
Wengine walieleza kuwa hawajawahi kuona beki anayefanya makosa kama Maguire.
“Tangu amewasili ametugharimu mabao mengi ya kufungwa, moja ya saini mbaya kuipata,” ilikuwa ni moja ya ujumbe.
Mbali na hivyo wapo ambao walikuwa wanamlinda ambapo wao walilikuwa wakisema:”Kama unatuonesha makosa yake tafadhali tuonyeshe na ujuzi wake na mabao hakuna haja ya kuweka maamuzi ya upande mmoja,”
Machi 6, Manchester United walifungwa mabao 4-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Etihad.
Ikiwa imecheza mechi 28 imefungwa jumla ya mabao 38 na ile ya ushambuliaji imetupia mabao 45 ikiwa nafasi ya 5 na pointi 47.