BAADA ya kikosi cha Yanga kusepa na pointi tatu mazima mbele ya Geita Gold Machi 6,2022 leo wanarejea Dar kikiwa na furushi la pointi kibindoni.
Bao pekee la ushindi lilijazwa kimiani na Fiston Mayele dakika ya 1 na lilidumu mpaka kipyenga cha mwisho.
Ushindi huo unaifanya Yanga iridium kujenga ngome kileleni ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 17.
Mayele anafikisha jumla ya mabao 10 kibindoni sawa na Relliants Lusajo ambaye ni mali ya Namungo FC inayotumia Uwanja wa Ilulu.