NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wale wanaosema kuhusu mchezaji wao mpya Chico Ushindi watamuelewa tu kwa sababu hakusajiliwa kwa makosa.
Chico ambaye ni ingizo jipya kwenye dirisha dogo mechi mbili za ligi amecheza na kutumia dakika 19.
Nabi amesema kuwa anasikia wengi wanazungumza kuhusu uwezo wa Chico na kwa nini hachezi hilo anajua na sababu zipo.
“Mashabiki wanauliza na wakiniona utasikia wananiambia Chico yuko wapi? Ninaweza kusema kwamba Chico yupo na atacheza kwenye mechi zijazo kwa kuwa ni mchezaji mzuri.
“Yeye hachezi kwa sasa kwa sababu hajawa fiti baada ya kupata maumivu lakini nimeona yupo vizuri na ameanza mazoezi hivyo muda ukifika ataonekana uwanjani na watamuelewa tu,” alisema Nabi.