BILIONEA Hansjorg Wyss raia wa Switzerland inaelezwa kuwa yupo kwenye hesabu za kuhitaji kuwa mmiliki wa Klabu ya Chelsea kwa kuwa anahitaji kuinunua baada ya habari kuelezwa kwamba Roman Abramovich yupo kwenye mpango wa kuiuza timu hiyo.
Bilionea huyo mwenye miaka 86 inaonekana kwamba anauhitaji wa kuwa mmiliki wa Chelsea inayotumia Uwanja wa Stamford Bridge ambayo ipo chini ya Abramovich lakini pia atakuwa na kampuni mbalimbali ambazo zinahitaji kuinunua timu hiyo.
Bilionea Abramovich ambaye alijiuzulu nafasi ya kuwa ndani ya uongozi wa bodi na kubaki kuwa mmiliki alikuwa na timu hiyo tangu 2003 yupo kwenye presha kubwa kwa sasa ya kuweza kufanya maamuzi ya kuweza kuuza umiliki wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.
“Abramovich anajaribu kuweza kuuza vitu vyake vyote vya gharama ambavyo vipo England,pia anataka kufanya hivyo katika suala la Chelsea haraka ,” Wyss ameliambia gazeti la Blick.
“Mimi na watu watatu tumepokea ofa ya kuinunua Chelsea kutoka kwa Abramovich nina paswa kusubiri sasa kwa muda wa siku nne ama tano kuanzia sasa kwa kuwa tumeipata ofa hiyo Jumanne lakini Abramovich kwa sasa anahitaji pesa nyingi,”