ABRAMOVICH ANATAJWA KUIWEKA SOKONI CHELSEA

BILIONEA Roman Abramovich inatajwa kwamba ameanza kuuza vitu ambavyo anavimiliki ndani ya England kwa bei ya hasara na anajaribu pia kuweza kuuza umiliki wa timu ya Chelsea kwa dau la euro bilioni 3 na milioni 200 kwa hofu ya kuweza kuzuiliwa vitu vyake kwa kuwa ni raia wa Urusi.

Miongoni mwa vitu ambavyo anamiliki na anahitaji kuviuza ni pamoja na nyumba za gharama na apartment kwa kuwa anahofia sheria na Serikali inaweza kuweka zuio kuhusu mali zake.

Abramovich anatajwa kuwa na utajiri wa 12.5 bilioni za kimarekani kwa mujibu wa Forbes na anamiliki Kensington mansion yenye thamani ya euro milioni 150,milioni 22 euro ni penthouse na pia ana ndege binafsi, helicopters 3 na magari imara na yale ya gharama  yanaotengenezwa Uingereza na dunia nzima kiujumla.

Pia anamiliki Klabu ya Chelsea ambayo ni ya gharama kubwa na iliweza kufanya usajili mkubwa ikiwa ni pamoja na kumuajiri Jose Mourinho pamoja na saini ya gharama kwa wachezaji kama Didier Drogba, hivyo kuiweka sokoni na kuiza Klabu ya Chelsea itakuwa ni pigo kwake kwenye masuala ya uchumi.