WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho, Simba leo Machi Mosi wamerejea Dar baada ya kukamilisha dakika 180 za msako wa pointi sita kimataifa ugenini.
Kwenye msako huo Simba iliambulia pointi moja na kufikisha pointi 4 kibindoni baada ya kupoteza mchezo mmoja wa kimataifa.
Ilikuwa mbele ya USGN ya Niger, Simba ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na mtupiaji alikuwa ni Bernard Morrison kwa pasi ya Shomari Kapombe ambaye alipiga kona.
Simba ilipoteza mbele ya RS Berkane kwa kufungwa mabao 2-0 hivyo iliyeyusha pointi tatu mazima na kuwafanya wapoteze mchezo wa kwanza katika hatua ya makundi msimu huu wa 2021/22.
Pablo Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wamerudi kwa ajili ya kujipanga kwa mechi zinazofuata ndani ya ligi pamoja na zilizobaki kwenye Kombe la Shirikisho.
“Tumerudi Tanzania tulikwenda kutafuta pointi tatu tumekosa lakini halikuwa kwenye mpango wetu, wakati ujao tutafanya vizuri na ni kwenye mechi zetu zijazo tutafanya kitu kupata pointi tatu muhimu,”.