NYOTA wa zamani wa Yanga, Tuisila Kisinda ambaye kwa sasa anacheza ndani ya kikosi cha RS Berkane ya Morocco amesema kuwa anaweza kurudi kwa mara nyingine Tanzania kucheza.
Kisinda alikuwa shuhuda wa ubao wa Uwanja wa Municipal de Berkane ukisoma RS Berkane 2-0 Simba na kazi kubwa ilifanywa na wachezaji wa timu ya RS Berkane ambao walipiga jumla ya mashuti 19 huku Simba ikipiga mashuti mawili pekee.
Kiungo huyo amesema:-“Yanga ni nyumbani na ninaipenda Yanga nimeimis Yanga, ninaipenda Yanga.
“Naongea tu Yanga ni nyumbani kama bosi ananitaka ninarudi nyumbani kucheza fresh tutaongea tu fresh.
“Fresh tu kwenye mpira hapa tunacheza na Tanzania tunaweza kucheza kwenye mpira fresh tu kila kitu kinawezekana,”.
Kiungo huyo alikuja Bongo pamoja na Tonombe Mukoko ambaye yeye msimu huu amejiunga na Klabu ya TP Mazembe.