UWANJA WA MKAPA YANGA V KAGERA SUGAR VITA YA KISASI

LEO Uwanja wa Mkapa itakuwa ni vita ya kisasi kwa Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu Francis Baraza v Yanga inayonilewa na Nasreddine Nabi katika mchezo wa mzunguko wa pili.

Yanga ni vinara katika mchezo wa kwanza walishinda bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba na mtupiaji alikuwa ni Feisal Salum ambaye leo ataukosa mchezo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi ya njano.

 Baraza raia Kenya amesema kuwa wanatambua Yanga ni timu imara na haijafungwa hivyo wataingia kwa tahadhari katika kujilinda na kushambulia.

“Mchezo wetu na Yanga utakuwa mgumu lakini timu itakayoweza kumiliki eneo la kati ina nafasi kubwa ya kushinda na kupata pointi tatu muhimu.

“Ninawaheshimu wapinzani wetu Yanga kwa kuwa wamekuwa na mwendo mzuri kucheza mechi 15 bila kufungwa hilo ni jambo kubwa,” amesema.

Nabi amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila amewaambia wachezaji wake wacheze kwa juhudi.

“Nimewaambia wachezaji wacheze kwa kujituma na wanajua kwamba tunahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa,”.

Mchezo wa mwisho kwa Yanga kukamilisha mzunguko wa kwanza ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu Ni Said Ntibanzokiza ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuwa alifunga na kutoa pasi ya bao kwenye mchezo huo.