MAYELE MWENDO WA MOJAMOJA BONGO

FISTON Mayele mzee wa kutetema dozi yake anayotoa kwa kuwatungua wapinzani wake ni mwendo wa mojamoja kwa kuwa hakuna timu ambayo ameifunga mabao Zaidi ya mawili.

Akiwa ametupia mabao 7 ni KMC walianza kutunguliwa na langoni alikuwa amekaa Faroukh Shikalo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Majimaji,Songea.

Azam FC ilikuwa timu ya pili kufungwa kisha ikafuata Mbeya Kwanza kisha biashara iliendelea mpaka walipokutana na Biashara United.

Dodoma Jiji walikutana na joto ya jiwe na hatua nyingine ikawa mbele ya Coastal Union ya Tanga na msumari wake wa 7 aliwatungua Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu Complex.

Hata kwa upande wa pasi bado ni mwendo wa mojamoja kwa kuwa alitoa pasi yake ya kwanza mbele ya KMC ilifungwa na Feisal Salum na ile ya pili alitoa mbele ya Polisi Tanzania ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania na mtupiaji alikuwa ni Dickson Ambundo.

Ndani ya Yanga inayoongoza ligi na pointi 39 amecheza mechi 15 ametumia dakika 1,161.