DICKOSN Ambundo,beki wa Yanga ni miongoni mwa nyota ambao wataukosa mchezo wa leo Februari 27 dhidi ya Kagera Sugar.
Job ambaye ni beki wa kati anaukosa mchezo wa leo kutokana na kuwa kwenye mwendelezo wa kutumikia adhabu ya kifungo cha mechi tatu ambacho alipata kutokana na kucheza mchezo usio wa kiungwana mbele ya Richardson Ng’odya wa Mbeya City.
Mbali na Job pia Feisal Salum atakosa mchezo kutokana na kuwa na adhabu ya kadi tatu za njano, kadi ya tatu aliipata mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kufunga bao la mkono.
Tatu ni Yacouba Songne huyu bado hajawa fiti pamoja na Chicho Ushindi ambaye huyu ni asilimia 50 kuanza ama kutoanza kwa kuwa alikuwa anaumwa.
Pia beki Abdalah Shaibu na Kibwana Shomari nao pia hawajawa fiti licha ya kuanza mazoezi kwa ajili ya kuweza kurejea kwenye ubora wao.
Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua kwamba wapo wachezaji ambao wataukosa mchezo wa leo lakini watawatumia wachezaji waliopo kupata matokeo.
“Chico ushindi yeye ni asilimia 50 anaweza kuanza ama kutoanza kwa kuwa hajawa fiti asilimia 100, hivyo mashabiki wanaweza kumuona akiwa benchi ama kuanza.
“Kwa wengine kama Kibwana,Job hawa hawatakuwa sehemu ya mchezo lakini Yassin Mustapha yeye yupo fresh,”.