POLISI TANZANIA KUKIWASHA LEO AZAM COMPLEX V KMC

MZUNGUKO  wa pili mdogomdogo kwa sasa unaanza leo Uwanja wa Azam Complex unatarajiwa kuchezwa mchezo kati ya KMC v Polisi Tanzania ambapo makocha wa timu zote mbili wameweka wazi kwamba wanahitaji pointi tatu.

Polisi Tanzania wameweka wazi kwamba wapo tayari kwa mchezo wa leo na wanahitaji pointi tatu muhimu.

George Mketo, Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya mchezo huo na wanataka pointi tatu muhimu.

“Wachezaji wote wapo imara na tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunajua kwamba tunakutana na timu ngumu lakini tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo ni Adam Adam atakosekana kutokana na matatizo ya kifamilia lakini wengine wapo tayari,” amesema Mketo

Polisi Tanzania imekusanya pointi 19 kwenye mechi zake 15 ambazo imecheza kwa mzunguko wa kwanza ipo nafasi ya 8.