HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga,amesema kuwa Uwanja wa Manungu ambao unatarajiwa kutumika leo kwa
mchezo wao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar kwao sio tatizo.
Yanga ambao ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 36, wanatarajia kukutana na Mtibwa Sugar iliyokusanya pointi 12 na zote zimecheza mechi 14.
Akizungumza na Championi Jumatano, Bumbuli alisema kila mechi wanazocheza kwao ni muhimu bila kujali wanacheza wapi kwa kuwa kikubwa ni pointi tatu.
“Mkulima mzuri yeye hachagui jembe kikubwa ambacho anaangalia ni namna gani anaweza kulitumia hivyo iwe ni Uwanja wa Manungu ama uwanja mwingine kwetu hakuna tatizo.
“Ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu kwani malengo yetu ni kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote,” alisema Bumbuli.