MORRISON ASIMULIA NAMNA ALIVYOFUNGA KIMATAIFA

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison mtupiaji wa bao lililoipa timu hiyo pointi moja amesema kuwa kwake ni furaha kufanya hivyo kwa ajili ya timu.

Ilikuwa jana Februari 20 Morrison akitokea benchi wakati Simba ikiwa ipo nyuma kwa bao 1-0 aliweza kuingia na kufunga bao.

Morisson aliingia dakika ya 64 akichukua nafasi ya Yusuph Mhilu kwenye mchezo huo wa makundi ukiwa ni mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa General Seyni Kountche.

Morrison amesema:”Nilikuwa uwanjani nikaona kwamba mpira umepigwa na ulikuwa unakuja kwangu sikuwa na jambo jingine zaidi ya kuupiga kuelekea golini,”.

Ilikuwa ni dakika ya 83 kona ilipigwa na mzawa Shomari Kapombe.