NGOMA iliyopigwa kiume katika hatua ya makundi imekamilika na kila timu kugawana pointi mojamoja.
Alianza Wilfred Gbeuli dk 11 kumtungua Aishi Manula kutokana na makosa ya safu ya kiungo na ulinzi ya Simba kufanya makosa.
Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco ilikwenda mapumziko ikiwa imetunguliwa bao moja na ilipiga shuti moja lililolenga lango kati ya matano.
Kiungo Bernard Morrison akitokea benchi ameweza kupachika bao dakika ya 83 na kuweka ubao wa Uwanja wa General Seyni Kountche kusoma 1-1.
Simba inafikisha pointi 4 na inaongoza kundi D kwa sasa na USGN wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi moja kibindoni.
Kituo kinachofuata ni RS Berkane, Morocco mchezo unaotarajiwa kuchezwa Februari 27.
RS Berkane ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 3 leo imepoteza mbele ya ASEC Mimosas kwa kufungwa mabao 3-1.