SIMBA KUYAKOSA MABAO 11 MAZIMA LEO KIMATAIFA

WAKIWA na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni wa makundi wawakilishi wa Tanzania, Simba watawakosa wachezaji wao watano ambao wamehusika katika kupatikana kwa mabao 11.

Ni mchezo wa pili dhidi ya USGN ya Niger katika kundi D baada ya ule wa kwanza dhidi ya ASEC Mimosas kuweza kushinda kwa mabao 3-1 na ulichezwa Uwanja wa Mkapa.

Nyota hao wanakosekana kutokana na sababu mbalimbali ni pamoja na kiungo Clatous Chama ambaye amerejea kwa mara nyingine akitokea RS Berkane ya Morocco ambaye alitupia bao moja kwenye ligi na manne kwenye Kombe la Shirikisho na kumfanya awe amefunga mabao matano huyu hayupo katika mashindano ya kimataifa msimu huu.

 Hassan Dilunga kiungo huyu anakumbukwa alifunga bao moja kwenye mashindano ya kimataifa ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Red Arrows kwa sasa anatibu jeraha la goti.

Kibu Dennis yeye alitupia mabao matatu kwenye ligi na bao moja kwenye Kombe la Shirikisho hivyo ana mabao manne kibindoni yupo Chris Mugalu bado hajatupia hawa bado hawajawa fiti.

 Mzamiru Yassin kiungo wa kazi ni bao moja alitupia kwenye mchezo wa ligi na Rally Bwalya alitupia bao moja kwenye mchezo wa ligi hawa wana matatizo ya kifamilia hivyo hawapo kwenye kikosi kilichopo Niger.