SIMBA KAMILI KUWAVA USGN YA NIGER KIMATAIFA LEO

AISHI Manula, kipa namba moja wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya USGN ya Niger.

Simba inakibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya USGN ikiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Timu zote zipo kundi D ambalo kinara ni RS Berkane mwenye pointi tatu akiwa na mtaji wa mabao matano aliyoshinda katika mchezo wa kwanza huku Simba ikiwa na pointi tatu na mabao matatu.

Mchezo wa kwanza Simba ikiwa Uwanja wa Mkapa iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas na kusepa na pointi tatu.

Manula amesema:”Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu tunaamini utakuwa mgumu lakini kwa maadalizi ambayo tumeyafanya na mbinu tulizopewa na mwalimu tunaamini tutapata matokeo.

“Sisi tulishinda mchezo wetu uliopita wenzetu wakapoteza na watakuwa nyumbani na sisi tunajua tukipata matokeo tutapata picha ya kile tunachokitafuta,”