BAO la kiungo mshambuliaji wa Simba, Pape Sakho limechaguliwa kuwa bao bora la wiki katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kiungo huyo alipachika bao hilo Februari 13,2022 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni kwa mtindo wa Acrobatic.
Alipachika bao hilo la ufunguzi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya ASEC Mimosas kwa kutumia pasi ya Shomari Kapombe ambaye anavaa jezi namba 12.
Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 ambapo mabao mengine yalifungwa na Kapombe na Peter Banda ambaye kutokana na kushangilia kwa kuvua jezi alionyeshwa kadi ya njano.