Klabu ya Simba leo Februari 10, 2022 imezindua rasmi jezi mpya ambazo zitakuwa zinatumika kwenye michuano ya kimataifa ambayo klabu hiyo ipo hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
“Leo tunaonyesha jezi yetu ya michuano ya kimataifa ikiwa na logo ambayo inazingatia mambo yote ya utalii.
Jezi zitaanza kuuzwa kesho kwenye maduka ya Vunja Bei na Sandaland The Only One.” amesema CEO Barbara.
“Jambo lolote ambalo lina maslahi kwetu kama Bodi ya Utalii lazima tulipe ushirikiano, lazima tulishangilie.
“Simba inapovaa jezi zimeandikwa Visit Tanzania imekuwa na faida sana. Kuvaa jezi hizo kumehamasisha Watanzania na kumekuwepo na ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi.”- Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo
Simba ipo Kundi D, ikiwa imepangwa pamoja na US Gendarmerie ya Niger na RS Berkane ya nchini Morocco
ambayo anaichezea Tuisila Kisinda.