KIBU DENIS, DILUNGA MAJANGA SIMBA

MENEJA Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefungukia maendeleo ya wachezaji wao Kibu Denis na Hassan Dilunga ambao kwa sasa ni majeruhi.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas utakaochezwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ally amesema: “Leo (jana) asubuhi Dilunga ameenda kuangaliwa tatizo lake na kujua ni kwa muda gani atakaa nje ya uwanja.

“Kwa upande wa Kibu, yeye bado hali yake siyo nzuri, ila Taddeo Lwanga amesharejea na kuanza

mazoezi na timu na huenda mwalimu akamtumia katika mchezo wa Jumapili.”