SALAH APANIA KULIPIZA KISASI KWA SENEGAL

MOHAMED Salah, staa wa timu ya taifa ya Misri amewasisitiza wachezaji wenzake kwamba watakwenda kulipiza kisasi mbele ya Senegal.

Ikumbukwe kwamba Salah alikuwa kwenye kikosi cha Misri kilichotinga fainali ya Afcon 2021 na kupoteza kwa kufungwa kwa penalti 4-2 baada ya dakika 120 kumeguka mazima.

Ni Sadio Mane wa Senegal ambaye alikosa penalti katika muda wa kawaida mepama kipindi cha kwanza aliweza kufunga penalti ya ushindi.

Baada ya Misri kukosa ubingwa wa Afcon 2021, Salah aliwasisitiza wachezaji wenzake kwamba watakwenda kulipiza kisasi watakapokutana uwanjani kwa mara nyingine tena.

“Tulicheza mechi nne zote dakika kwa dakika 120 ndani ya takribani siku 12, lakini yamepita sasa tuna mechi dhidi yao mwezi ujao na tuombe uzima tutalipiza,”.

Misri na Senegal zinatarajia kukutana katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwezi ujao huku timu itakayoshinda ikipata nafasi ya kuwa moja ya timu tano zitakazoiwakilisha Afrika katika michuano hiyo.

Mechi ya kwanza itachezwa Cairo, Machi 23 kabla ya mchezo wa marudiano jijini Dakar,Machi 29.

Tayari Salah amerejea katika timu ya Liverpool kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ushindani.