MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele amecheguliwa kuwa mchezaji bora kwa mwezi Januari baada ya kuchaguliwa na Kamati ya Tuzo za TFF iliyokutana wiki hii Dar.
Mayele mwenye mabao sita na pasi mbili za mabao amekuwa ni mshambuliaji mwenye mwendo bora awapo uwanjani na ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji wengine ambao aliingia nao fainali ikiwa ni pamoja na Relliats Lusajo wa Namungo pamoja na kiungo Tepsi Evans wa Azam FC.
Mayele anakuwa ni mchezaji wa tano kutwaa tuzo hiyo ambapo wengine ambao walitwaa tuzo hiyo ni pamoja na Lusajo wa Namungo kwa Desemba, Jeremia Juma mshambuliaji wa kwanza kufunga hat trick wa Tanzania Prisons aliwafunga Namungo alitwaa tuzo hiyo Novemba.
Feisal Salum wa Yanga alitwaa tuzo hiyo Oktoba na Vitalis Mayanga wa Polisi Tanzania ambaye alikuwa mshambuliaji wa kwanza mzawa kuanza kufunga mabao mawili kwenye mchezo mmoja ilikuwa mbele ya KMC alitwaa tuzo hiyo Septemba.