KIUNGO mshambuliaji wa Kimataifa raia wa Ghana, anayekipiga ndani ya Klabu ya Simba, Bernard Morrison amemamisha kwa muda hadi suala lake la kinidhamu litakapo patiwa ufumbuzi.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya klabu hiyo, Morrison amekuwa na tabia ya kutoka kambini bila ruhusa kinyume na taratibu
Aidha ametakiwa kutoa maelezo ya maandishi kwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na akishindwa kufanya hivyo hatua zaidi za kinidhamu zitachukuliwa.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wake wa zamani Yanga wameweka malengo ya kuinasa kwa mara nyingine tena saini yake.
Ikumbukwe kwamba Morrison aliachana na Yanga Agosti 8,2020 kisha akatambulishwa ndani ya Simba ambapo kwa sasa mkataba wake unakaribia kufika ukingoni.