LEO Februari 4,2022 timu ya taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzanite itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya Ethiopia.
Hii ni mechi ya pili ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.
Katika mechi ya kwanza mjini Zanzibar wiki mbili zilizopita, Tanzanite waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mechi ya leo ni ushindi au sare kwa Tanzanite na ikipoteza hali itakuwa ngumu kwa Tanzanite kuweza kupenya katika Kombe la Dunia.
Kocha Mkuu wa Tanzanite, Bakari Shime amesema wana imani wanapambana kuhakikisha wanasonga mbele kuwania kucheza Kombe la Dunia.
“Itakuwa ni mechi ngumu lakini tumefanya maandalizi bora tukiwa Karatu,tunaamini makosa tuliyofanya Zanzibar tumeyarekebisha na tutapambana kupata ushindi,”.