SIMBA QUEENS KUVAANA NA JKT QUEENS LEO

SIMBA Queens leo Februari 4 inatarajiwa kuwa na mchezo wa kusaka pointi tatu mbele ya JKT Tanzania.

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Bunju Complex.

Ni saa 10:00 jioni mchezo unatarajiwa kuchezwa kwa kila timu kusaka pointi tatu muhimu.

Simba Queens mchezo wake uliopita ilikuwa dhidi ya Mlandizi Queens na iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 ilikuwa katika Uwanja wa Bunju Complex.

Ikumbukwe kwamba Simba Queens ni mabingwa watetezi wa taji hilo.