>

KILICHOPANDWA KIMEVUNWA KOMBE LA SHIRIKISHO

MATUKIO ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi uwanjani yapo yanayokera na yanayofurahisha lakini muhimu kila mmoja kuwa makini katika kutekeleza majukumu yake.

Tumeona kwamba kuna wachezaji ambao wamekuwa wakitumia nguvu kubwa nah ii inatokana na hasira lakini kwa namna yoyote ile ni lazima kila mchezaji kuwa mlinzi wa mchezaji mwenzake.

Kwa timu ambayo itakosa kupata matokeo haina maana kwamba haijafanya maandalizi mazuri bali ni makosa ambayo wanayafanya kwenye uwanja.

Tumeshuhudia namna Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora mambo yalivyokuwa na ambacho kimevunwa ni kile ambacho kimepandwa kwa timu husika.

Yote kwa yote zile ambazo zimesonga mbele hatua ya 16 bora zinastahili pongezi na kujipanga kwa mechi zijazo.

Masuala ya usajili tayari majalada yake yamefungwa na kilichobaki kwa sasa ni kazi juu ya kazi hakuna namna nyingine.

Jambo kubwa na muhimu la kufanya kwa wakati huu ni maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi zijazo kwa kuwa mwisho wa kazi moja ni mwanzo wa kazi nyingine ngumu.

Napenda pia kuwapa pongezi mashabiki ambao wanajitokeza kushangilia timu zao wameonekana kuwa na nidhamu jambo hili ni kubwa na zuri kwa wanamichezo.

Imani yangu ni kwamba kwa wale ambao wamekuwa na tabia ya kubeba matokeo mfukoni wanashuhudia kile ambacho wanakipata baada ya dakika 90.

Wachezaji pia nimeona namna ambavyo wanacheza kwa nidhamu kubwa katika kutimiza majukumu yao nao pia wanastahili pongezi.

Makosa ambayo wanayafanya kisha wapinzani wao wakashindwa kuyatumia wanakazi ya kuweza kufanyia maboresho wakati ujao ili kuwa imara zaidi.

Ipo wazi kwamba kuna ulazima wa wachezaji kufanya maandalizi mazuri na kuwa vizuri kisaikolojia kwa ajili ya matokeo ambayo yatapatikana baadaa ya dakika 90.

Kila timu inashangaa namna ambavyo inapata matokeo lakini hakuna muda wa kushangaa kwa sasa ni muda wa kazi mwanzo mwisho.

Raundi ya 16 ipo njiani kuja jambo la muhimu ni kuweza kujipanga kwa kila mmoja ili aweze kupata kile ambacho anastahili.

Katika  hili ni muhimu wachezaji kutambua kwamba malengo ya timu yapo ili yaweze kutimizwa na wanaopaswa kuyatimiza ni wachezaji wenyewe.

Kwa namna yoyote ile kwenye mashindano ambayo timu zinashiriki hesabu kubwa ni kupata ushindi hivyo ili kushinda ni muhimu kuweza kupambana kupata kile ambacho.

Haya ni mashindano makubwa na yanahitaji kupewa kipaumbele kwa kila timu shiriki ili kupata ushindi hasa ukizingatia kwamba kuna zawadi pamoja na kuweza kushiriki katika mashindano ya kimataifa.

Hili ni daraja kwa timu shiriki kuweza kuibeba nchi kimataifa na ili iwezekane kuwa hapo lazima kupambana kwa hali na mali katika kusaka ushindi.

Waamuzi ambao watapewa majukumu ya kusimamia mashindano haya kazi yao iwe moja kufuata sheria 17 za soka kwa kuwa wakifanya hivyo kila kitu kitakwenda sawa.

Yale malalamiko ambayo yamekuwa yakitokea kwenye mechi za ligi basi yanapaswa yapunguzwe na kufanyiwa kazi kabisa huku kwenye kombe la Shirikisho. Basi kila la kheri wachezaji na waamuzi ambao wanasimamia mashindano haya kila kitu kinawezekana.