>

MUGALU NA BOCCO WATOA GUNDU SIKU YA 193

JANUARI 28 mastaa wawili wa Simba ambao ni washambuliaji, John Bocco na Chris Mugalu walitoa gundu ya kutofunga kwa muda mrefu kwenye ligi kwa kuweza kufunga kwenye mazoezi.

Ilikuwa ni siku yao ya 193 ya kuweza kucheza bila kufunga baada ya kuweza kutupia mara ya mwisho Julai 18,2021 katika mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC.

Wawili hao walifunga mabao kwenye mazoezi ya timu hiyo ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Dar City kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Bunju.

Bocco alifunga bao moja kwa kichwa akitumia krosi iliyopigwa na Pape Sakho na Mugalu pia alifunga bao kwa pasi ya Pape kwa kichwa ndani ya 18.

Pia Mugalu alifunga bao akiwa kwenye mwendo baada ya kukokota mpira akiwa nje ya 18 na kufunga kwa shuti lililomshinda kipa Aishi Manula.

Leo saa 1:00 usiku watakuwa na kazi mbele ya Dar City mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora.