VIDEO:KOCHA WA SIMBA PABLO AFUNGUKA KUHUSU KUSHINDWA KUPATA USHINDI

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wameshindwa kupata ushindi kwenye mechi zao ambazo wamecheza kutokana na kushindwa kuzitumia nafasi ambazo wamezipata na wanamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mechi zao zijazo.

Simba imeshindwa kupata ushindi kwenye mechi tatu ambapo ilikuwa mbele ya Mbeya City ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar ililazimisha sare ya bila kufungana na mbele ya Kagera Sugar ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.