YANGA:LIGI NI NGUMU,TIMU ZOTE ZIMEJIPANGA

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ligi sio nyepesi kwa kuwa kila timu imejipanga kupata pointi tatu.

Kwenye msimu wa 2021/22 mpaka sasa Yanga haijapoteza mchezo hata mmoja baada ya kucheza mechi 10 ikiwa imeshinda nane na kulazimisha sare mechi mbili.

Mchezo wake uliopita ilikuwa mbele ya Biashara United ambapo ilishinda mabao 2-1 na kusepa na pointi tatu mazima.

Nabi amesema:”Ligi ni ngumu na hakuna mchezo mwepesi ambao tunakutana nao hilo lipo wazi kwa kuwa kila timu ambayo tunakutana nayo inahitaji ushindi.

“Kikubwa ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya nasi kwani ili uweze kupata pointi hakuna namna nyingine unayotakiwa kufanya zaidi ya kushinda,”.