>

YANGA:TUNAKAMIWA KWENYE MECHI ZETU

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema licha ya kuibuka na ushindi 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons, kikosi chake kinakutana na wakati mgumu kwani kila timu wanayokutana nayo inacheza kama fainali dhidi yao.

Yanga imefikisha pointi 23 na kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikifuatiwa na Simba yenye pointi 18 na mchezo mmoja pungufu.

Nabi ameweka wazi kwamba kwenye mchezo wao dhidi ya Prisons walikuwa hawana namna ya kufanya zaidi ya kusaka ushindi licha ya kwamba wachezaji wake wengine walikuwa ni wagonjwa.

“Kuna wachezaji wetu muhimu walikuwa wagonjwa lakini walisema watacheza na kupambana kwa ajili ya mashabiki ambao wamekuwa wakiwasapoti na wataipigania Yanga na ndivyo walivyofanya, kama kocha napenda kuwapongeza.”

“Kila timu inapocheza na Yanga inacheza kama fainali hivyo tunajiandaa kwani tunajua kila mchezo unakuwa mgumu na wachezaji wanaelewa hilo,” alisema Nabi.

Kwa sasa Yanga ipo kwenye maandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Biashara United ya Mara unaotarajiwa kuchwezwa Uwanja wa Mkapa Desemba 26.

Miongoni mwa wachezaji ambao walianza kikosi cha kwanza na kufanya kweli ni pamoja na Feisal Salum ambaye alipachika bao moja pamoja na Khalid Aucho aliyepachika bao la ushindi kwa pasi ya Said Ntibanzokiza huku lile la Prisons likifungwa na Samson Mbangula.