MAKAMBO ATAJA SABABU YA KUTOFUNGA,ASHUSHA PRESHA

HERITIER Makambo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa sababu ya kushindwa kufunga ndani ya Ligi Kuu Bara kwa wakati huu ni kutokana na muda kutofika ila ukifika atafunga tu.

 

Nyota huyo kwa msimu wa 2021/22 Yangaikiwa imecheza mechi 7 ndani ya ligi na yeye akicheza katika mechi tano hajaweza kufunga bao wala kutoa lasi pia ya bao.

 

Makambo amesema , “Najua mashabiki wanahitaji kuona nikifunga, muda bado nitafunga tu ni jambo la kusubiri,muda ukifika nitafunga hata mimi pia napenda kufunga.

 

“Kila kitu kina wakati wake kwa sasa nina amini kwamba nitafunga muda wangu ukifika na nitafanya vizuri lakini ninachofurahi ni kwamba timu inapata matokeo,”.

Yanga ipo nafasi ya kwanza katika msimamo na pointi zake ni 19 kibindoni inafuatiwa na Simba iliyo nafasi ya pili.

 

Imefunga jumla ya mabao 12 na vinara ni wawili ambao ni Feisal Salum na Fiston Mayele wote wametupia mabao matatumatatu.

 

Baada ya kumalizana na Mbeya Kwanza, kituo kinachofuata ni Desemba 11 dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa.