DUH! RONALDO AAMBIWA NI MZEE SANA

MASHABIKI wa Manchester United wameanza kuwa na hofu kubwa siku chache kabla kocha mpya hajaanza kufundisha timu hiyo ambayo jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

United inatarajiwa kufundishwa na kocha Ralf Rangnick ambaye anatarajiwa kukaa kwenye timu hiyo hadi mwisho wa msimu wa 2021/22.

Kocha huyo raia wa Ujerumani anatarajiwa kuanza kuifundisha timu hiyo kuanzia kwenye mchezo ujao ambapo hofu ya mashabiki hao ni kama ataweza kumtumia mchezaji Cristiano Ronaldo kwa kuwa aliwahi kumuita mzee.

Akiwa nchini Ujerumani kocha huyo mwenye mbwembwe za kutosha aliulizwa na Waanidhishi wa Habari kama yupo tayari kumsajili mmoja kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambapo alijibu kwamba hawezi kufanya hivyo.

“Siwezi kumsajili Ronaldo kwenye timu yangu kwa kuwa ni mchezaji mzee sana na hawezi kucheza kwenye mfumo wangu,” alisema kocha huyo.

Kauli hii imeanza kuwapa hofu mashabiki wa United kwa kuwa wanaamini kwamba kama kocha huyo alisema hivyo wakati Ronaldo akiwa na miaka 30 sasa itakuaje wakati kwa sasa nyota huyo ana miaka 36.