WANANCHI NI MWENDO WA USHINDI TU HUKO

WANANCHI wameendelea kuwa na furaha baada ya kushinda mabao 2-1 mbele ya KMKM FC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Wamekuwa kwenye mwendo wa ushindi kwa kuwa hata mchezo wa kwanza walipocheza dhidi ya Mlandege, Yanga ilishinda bao 1-0 na mtupiaji alikuwa ni Heritier Makambo ilikuwa ni Novemba 9.

KMKM FC walikuwa wa kwanza kupachika bao kupitia kwa Optatus Lupekenya ambaye alitumia mpira wa makosa ya Abdallah Shaibu,’Ninja kisha Lupekenya akawatungua Yanga katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Jesus Moloko alisawazisha bao dakika ya 27 akitumia pasi ya Deus Kaseke aliyoitoa kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 huku Moloko akiwa ndani ya 18 na kupachika bao hilo kwa kichwa kilichomshinda kipa Nassoro Abdallah Nassoro.

Chuma cha pili ilikuwa kazi ya Fiston Mayele dakika ya 85 kwa pasi ya Yannic Bangala ambapi alipachika bao kwa mtindo wa kubinuka,tikitaka safi baada ya Moloko kupiga kona ya moja kwa moja katika mchezo huo wa kirafiki.