TIMU ya Taifa ya Tanzania,Taifa, Taifa Stars kesho ina kibarua kingine cha kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Madagascar katika mchezo wa kuwania Kufuzu Kombe la Dunia.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Novemba 14 na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote kwa sasa hazina cha kupoteza zaidi ya kutafuta heshima.
Jana Novemba 13 Stars ilisepa Tanzania na Serikali kupitia kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa iliweza kuendelea kutoa sapoti na Bashungwa alipata muda wa kuzungumza na wachezaji wa Timu ya Taifa,Taifa Stars, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kuelekea Madagascar kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.
Matumaini ya Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen kufuzu Kombe la Dunia yaliyeyuka baada ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya DRC Congo kwenye mchezo uliochezwa Novemba 11, Uwanja wa Mkapa.
Katika msimamo kwa sasa Stars ipo nafasi ya tatu na pointi zake ni zilezile ambazo ziliweza kuifanya ia kushika nafasi ya kwanza kwa muda ambazo ni 7.
DR Congo ambao walikuwa nafasi ya tatu wakati huo kwa sasa wapo nafasi ya pili na pointi 8 huku nafasi ya kwanza ikiwa mikononi mwa Benin ambao wana pointi 10.
Madagascar wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi zao tatu kwenye mechi tano wao walishinda mchezo mmoja na mingine minne walipoteza ila sio wa kuwachukulia poa ni moja ya timu imara.