>

MASHABIKI WAITWA,DR CONGO WAANZA KUJA KWA MAFUNGU

WILFRED Kidao Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania,  (TFF ) amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya DR Congo yapo vizuri na wanaamini kwamba watafanya vizuri katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.

 

Novemba 11,2021, Stars ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya DR Congo katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapaa saa 10:00 jioni.

Kidao amesema:”Maandalizi yanakwenda vizuri na kila mchezaji yupo sawa kikubwa ni kuona kwamba mashabiki wanajitokeza kwa ajili ya mchezo wetu kwa kuwa hao ni wachezaji wa 12.

“Kiingilio ni rafiki hasa ukizingatia kwamba tumeweza kupata vigezo vile kwa ajili ya kupata watazamaji hilo inamaanisha kwamba bado tunatakiwa kuendelea kufuata taratibu kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Corona.

“Kwa upande wa wachezaji wa DR Congo wameanza kuja kwa mafungumafungu hivyo tunaendelea kuwapokea kwa ajili ya mchezo wetu ambao ni muhimu kwa ajili ya kupata ushindi na namna ambavyo tunapata sapoti kutoka kwa Serikali  ni jambo ambalo linatuongezea nguvu,” amesema.

Wachezaji chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen wameendelea kufanya mazoezi Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya mchezo huo wa kundi J ambapo Stars inaongoza kundi ikiwa na pointi 7 sawa na Benin yenye pointi saba huku DR Congo ikiwa nafasi ya tatu na ile ya nne ipo mikononi mwa Madagascar.