BREAKING:SIMBA YAMTANGAZA MRITHI WA GOMES NI KUTOKA HISPANIA

KLABU ya Simba leo Novemba 6 imemtangaza rasmi Pablo Franco mwenye miaka 41 kuwa mrithi wa mikoba ya Didier Gomes ambaye alibwaga manyanga kutokana na timu hiyo kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Franco ni raia wa Hispania anachukua mikoba ya Gomes ambaye ni raia wa Ufaransa na alisitisha mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Kabla ya kuibuka ndani ya Simba alikuwa anaifundisha Al Qadsia SC ya Quwait kuanzia 2019 hadi 2021.

Kocha huyo amesaini dili la miaka miwili kwa ajili ya kuwa ndani ya kikosi hicho cha Simba ambacho kipo nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 11 baada ya kucheza mechi tano.