BAADA ya Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo kushindwa kuanza katika mchezo hata mmoja kikosini hapo msimu huu, kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ameweka wazi sababu za nyota huyo kushindwa kupenya kikosi cha kwanza.
Makambo tangu atue Yanga msimu huu, ameshindwa kupenya katika kikosi cha kwanza katika michezo mitano ya ligi kuu, huku akimuacha Fiston Mayele akitamba.
Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Nabi alisema sababu kubwa ya Makambo kushindwa kucheza ni kutokana na ubora unaozidi kuoneshwa na Mayele ambaye ameonesha kuwa fiti tofauti.
“Makambo atacheza tu katika michezo ijayo kwani kuna michezo mingi mbele, lakini kwa sasa kilichotokea kinafahamika, timu ya ushindi huwa haibadilishwi mara kwa mara, Mayele anafanya vizuri sana ndio maana anatumika zaidi kuliko Makambo
“Lakini pia ukiangalia kuna sheria ya kutumia wachezaji nane wa kimataifa kwenye mechi moja, hivyo wakati mwingine naye ataonekana,” alisema kocha huyo.