LIGI Kuu Tanzania Bara kwa sasa imezidi kuwa ya moto kutokana na kasi ya timu zote kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.
Mabingwa mara 27 Yanga bado ni namba moja wakiwa na pointi zao 15 wanafuatiwa na Simba wenye pointi 11 kibindoni na wote wamecheza mechi tanotano.