MAYELE ATAJA IDADI YA MABAO ANAYOTAKA KUFUNGA

FISTON Mayele, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa hesabu zake kubwa ni kuona kwamba anaweza kufunga mabao kuanzia 20 jambo ambalo litaipa timu hiyo mafanikio.

Kwa sasa mshambuliaji huyo ametupia mabao mawili kwenye ligi aliwafunga KMC na Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mayele amesema kuwa anafurahi kufunga na anatarajia kufunga mabao mengi zaidi ya aliyofunga alipokuwa nchini DR Congo.

“Nahitaji kufunga mabao mengi na ninataka kufunga zaidi ya yale ambayo nilifunga nilipokuwa DR Congo hivyo kikubwa ni kuona kwamba ninaweza kufunga zaidi.

“Mabao ya kufunga kuanzia 20 ninafikiria kufunga ili kuweza kuipa mafanikio timu yangu na inawezekana kwa kuwa tumekuwa na ushirikiano mkubwa,” .